July 7, 2021


 ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC ya Mbeya amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zao ambazo zimebaki ili kupata matokeo chanya.

Ikiwa imecheza mechi 32 ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 35 kibindoni, katika nafasi ambayo ipo ni nyekundu kwake kwani ikipoteza mechi zake zilizobaki inaweza kushuka mazima mpaka Ligi Daraja la Kwanza. 

Ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Julai 14 ambapo ule wa awali Uwanja wa Sokoine ulikamilika kwa ubao kusoma Ihefu 0-3 Yanga.

 Katwila amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata ushindi hivyo watapambana ili kufanya vizuri.

"Kila timu inahitaji kupata matokeo hata sisi pia tunahitaji kushinda, jambo la msingi ni kuona tunapata matokeo hivyo bado kazi inaendelea.

"Mashabiki watupe sapoti kwa kuwa nao wana nguvu na nafasi katika kuyasaka mafanikio yetu kila kitu kinawezekana na imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic