WAKATI leo Julai 7 Klabu ya KMC ikitarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Simba, mabosi wa timu hiyo wamefungukia ishu ya kudaiwa kumkodi Haji Omari Mpili, maarufu kama Mzee Mpili.
Jana, Julai 6 ilisambaa twiter iliyokuwa inaonesha kwamba inamilikiwa na Klabu ya KCM ambayo ilisomekana namna hii:”Tumemkodi kwa muda Mzee Mpili, mtajua amjui,”.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa akaunti hiyo sio yao na wala hawana mpango wa kufanya hivyo.
"Hiyo akaunti siyo yetu na hatuijuia kabisa kwa kweli, hatuna mpango wa kufanya hivyo vijana wetu wapo vizuri na maandalizi yapo sawa," .
Mzee Mpili amekuwa akitamba kwamba ushindi wa Yanga walioupata Julai 3 wa bao 1-0 dhidi ya Simba ni yeye alikuwa mchezaji namba moja jambo ambalo lilifanya KMC wadai kwamba nao watamkodi kwa muda.
Mpili alisikika akisema kuwa:"Ushindi wa Yanga mimi nilikuwa mchezaji namba moja hivyo hakukuwa na namna kwa Simba kutufunga ilikuwa lazima wafungwe kwa kuwa mimi nina watu," .
Huyu mzee anaturudisha nyuma kisoka,, wenzake tushapiga hatua ndiyo maana ht kambi kabla ya derby huckii tena zanzibar wala bagamoyo! Mzee anataka turudi soka la miaka ya 70-90
ReplyDeleteUsiumize kichwa na kuuchosha ubongo wako kwa kuamini habari za vijiweni kama hizi.Tofauti iliyopo ni njia za uwasilishaji tu,either kupitia mtandaoni kama hii au physically meeting/gathering
DeleteNdio faida ya kuabudu na kupromote ushirikina, soka letu liko mashakani, wakulaumiwa ni utopolo na waandishi takataka
ReplyDeletePia usisahau habari za wafuga paka na manyau yao!!
Delete