July 17, 2021


 MANCHESTER United ipo kwenye hesabu za mwisho kukamilisha kupata saini ya beki Raphael Varane wa Real Madrid na Kieran Trippier kutoka Spurs.

United hawakuwa vizuri kwenye safu ya ulinzi msimu uliopita na sasa wanataka kuhakikisha kwamba wanakuwa na timu bora.

Inaelezwa kuwa inaweza kutumia jumla ya kitita cha pauni milioni 140 kwa ajili ya mastaa hao wakichanganya na kitita walichotumia kuipata saini ya Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund.

Kwa ajili ya mabeki hao wawili United watatumia kitita cha pauni milioni 68 kwa ajili ya kuwapata wachezaji hao. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic