July 24, 2021

 


BAADA ya kusajiliwa na Azam FC, beki kisiki, 
Edward Manyama, amesema kuwa ilikuwa ni ndoto yake kuichezea timu hiyo tangu akiwa JKT Tanzania, Namungo hata Ruvu Shooting.


Nyota huyo amesajiliwa na Azam akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Ruvu Shooting kumalizika mwishoni mwa msimu.


Manyama alitambulishwa Jumanne baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’.


Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo

alifunguka: “Ilikuwa ndoto yangu kuichezea timu ya Azam FC tangu nikiwa JKT Tanzania, Namungo na Ruvu Shooting.


“Naushukuru uongozi wa Azam kwa kunisainisha mkataba huu naahidi kujituma na kujitolea kwa bidii ili klabu yetu iweze kufanya vizuri.”


Nyota huyo anaungana na nyota wengine watano ambao ambo ni wapya kwa ajili ya kutimiza majukumu ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Anakuwa ni mzawa wa kwanza kutambulishwa ndani ya Azam FC kwa kuwa wengine ambao walitambulishwa ikiwa ni pamoja na Charles Zulu na Rodgers Kola kutoka Zambia, Keneth Muguna kutoka Kenya na Paul Katema naye wa Zambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic