July 24, 2021

 


KOCHA wa Makipa wa Yanga, raia wa Kenya,

Razack Siwa, amefungukia ishu ya kuhitajika

kwa mrithi wa Metacha Mnata kwa kusema

kuwa, hadi muda huu hajashirikishwa lolote juu ya usajili zaidi yeye ametakiwa kujikita kwenye masuala ya ufundi tu.


Tangu Metacha aliporipotiwa kusimamishwa na

klabu hiyo kwa tuhuma za utovu wa nidhamu,

mwezi uliopita, mabosi wa Yanga walikaririwa

wakisema wapo kwenye hatua za kutafuta

golikipa mpya wa kimataifa.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha wa

Makipa wa Yanga, Siwa alisema kuwa, hadi

muda huu yeye hana taarifa sahihi juu ya

viongozi kusajili kipa mpya, pamoja na kuwepo

na hitaji hilo.


“Kusema kweli taarifa za kuongeza kipa mpya

nimezisikia tu, ila mimi sijui lolote ni wapi

anatoka na atakuja lini, hivyo kazi yangu kwa

sasa mimi nimejikita kwenye kufundisha na kama kuna hilo basi tutajua huko mbeleni,”

alisema Siwa.

2 COMMENTS:

  1. C mlisema kipa kutoka nchi gani cjui, rasmi yanga au mlikuwa mnaota

    ReplyDelete
  2. Wasikilizeni waandishi kama kawaida ya watu wenye mihemko ya mikia kupinda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic