July 17, 2021

MSHAMBULIAJI Fiston Mayele kutoka katika klabu ya AS Vita amefunguka kuwa wiki ijayo atatua nchini kwa ajili ya kukamilisha usajili wake rasmi wa kujiunga na Yanga akiwa sambamba na beki wa kulia Shabani Djuma.

Djuma yeye ameshakamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga huku Mayele yeye akibakisha baadhi ya mambo ili aweze kujiunga na timu hiyo.

Akizungumzia kuhusu mipango yake ya kujiunga na Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa wiki ijayo anatarajia kutua nchini Tanzania kukamilisha usajili wake wa kujiunga na timu hiyo mara baada ya kusaini makataba wa awali wa miaka miwili, na uongozi wa Yanga ambao tayari wameshatuma tiketi za kuja nchini akiongozana na Shabani Djuma. 

“Nimezungumza na bosi wa Yanga tayari na wiki ijayo natarajia kuja Tanzania kukamilisha taratibu zangu zote za usajili, katika mkataba ule wa awali ambao tulikubaliana na Yanga ulikuwa ni wa miaka miwili na mambo mengine yatamalizika huko pindi nikifika kwa mujibu wa viongozi wa Yanga.

“Yanga wameniambia kuwa nitakuja Tanzania nikiwa na Shabani Djuma wiki ijayo, na tayari wameshatuandalia tiketi zetu kuhusu mkataba wangu na AS Vita ulishafikia ukingoni mwisho wa msimu huu na sababu iliyofanya nishindwe kuongeza mkataba pale ni kuwa na ofa nyingi ikiwemo ya Yanga ambayo imenivutia sana,”

Fiston Mayele msimu huu akiwa na klabu ya AS Vita katika ligi kuu ya nchini DR Congo amefanikiwa kumaliza akiwa mfungaji namba mbili mara baada ya kufanikiwa kutupia jumla ya mabao 13.

10 COMMENTS:

  1. Anatoka Fiston anaingia Fiston, what a coincidence!

    ReplyDelete
  2. Hahahaaaa umenichekesha na comment yko bro kwakwel hilo jina linanipa mashaka ata mm japo ni shabiki wa yanga

    ReplyDelete
  3. Hakuna ujinga unazidi kulalili kuliko kuelewa

    ReplyDelete
  4. Shida Ni mwenye Blog yeye na Haji Manara zao moja ,ok tetesi lkn kujaa na kupwa,Yanga hata akija huyo zingatia tuna unwanted men Nchimbi na Yacouba Hawa wengine Ni Ziada ,waulize Achieng na Wawa walilamba ardhi kwa motion za kiume mtalia tu ,bt also zingatia Fiston Ni sawa tu mhde. kagere /Mohamed hiyo mbona nyingi mbona unakwazika na Fiston????

    ReplyDelete
  5. Ac Vita ya Bongo iliyojaa wacongoman hahaha

    ReplyDelete
  6. AS Vita imefungua tawi bongo, linaitwa AS utopolo. Mara paaa yanga anapangwa k7ndi moja na vita kwenye mechi za caf, nini kitatokea

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mikia vipi.... Nyie hamkuliwaza Hilo kipindi mnawachukua akina onyango, kagere na kahata

      Delete
  7. Iwe As vita ana tawi huku bongo fresh ila nyie Mikia mshasahau kuwa hata For mahia ni ana tawi pale msimbazi embu tulizeni hivyo vipila bhas mbona mna mihao isiyo kuwa ya kawaida

    ReplyDelete
  8. Replies
    1. Yanga juuuu big up , acha waseme watalala,akifika NDio mtamjua usimseme haka fika Badae muumbuke

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic