July 17, 2021


 SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Namungo ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo ni wa mwisho kwa msimu wa 2020/21 ambapo Simba ni mabingwa wa msimu wa 2020/21 wanakutana na Namungo FC ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco.

Inakuwa ni mara ya pili kwa Simba kukabidhiwa ubingwa mbele ya Namungo FC kwa kuwa hata msimu uliopita wa 2019/20 ilikuwa hivyo walipocheza Uwanja wa Majaliwa na dk 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.

Matola amesema:"Tunajua kwamba mchezo wa kesho utakuwa mgumu na tupo tayari kwa ajili ya kuona kwamba tunapata ushindi hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti.

"Tuna bahati ya kupewa kombe mbele ya Namungo kwa kuwa mchezo uliopita tulilazimisha sare ya bila kufungana kwao ila safari hii wanakuja nyumbani hivyo ni suala la kusubiri na kuona.

"Kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu kwa kuwa hatuwezi kuona kwamba tunakabidhiwa kombe bila kuwa na furaha mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.

Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein amesema kuwa ni furaha kwao kuchukua ubingwa mara ya nne na wanafurahi kuona kwamba wanavaa medali ya nne. 

5 COMMENTS:

  1. Lakini isiwe wote wa kikosi cha kuwajaribu wasiopata nafasi kwani nao timu ngumu wakiiuumiza yanga

    ReplyDelete
  2. Wao wameshatamka wataichapa Simba

    ReplyDelete
  3. Mna bahati na Namungo au mna bahati na Tawi lenu?

    ReplyDelete
  4. Wapi PM??? Nasikia alipiga thiiiiimu

    ReplyDelete
  5. Hii Namungo, KMc, Coastal,Biashara,Mbeya City,Ihefu,Azam b4 Lwandamina,..JKT,Kagera,na Dodoma Jiji Ni Wachezaji kugawanyika by wengi Tawi lenu Wanacheza chini ya Kiwango.zile sita za kwanza wapo tayari kufungwa ,fungu la Pili 50@ nisizo taja zilipambana kwa uwezo wao Sasa eleza we mkia ,usisahau marefa na board ya Ligi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic