July 17, 2021

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa baada ya kustafu kucheza ndani ya Yanga angependa kuona jezi yake namba nane ikivaliwa na kiungo Zawadi Mauya, huku Feisal Salum akimuomba Niyonzima amkabidhi namba hiyo kama atapenda.

Mauya ambaye ni kiungo makabaji wa timu hiyo kwa sasa, ndani ya Yanga anavaa jezi namba 20 huku Feisal Salum akiwa anavaa jezi 6.

Akizungumzia kuhusu jezi yake ndani ya Yanga Niyonzima amesema: "Natamani kuona Zawadi Mauya akivaa jezi yangu namba 8 mara baada ya mimi kustaafu, sababu kubwa ni uwezo wake Pamoja na jitihada ambazo amekuwa akizionyesha ndani ya Uwanja, nakumbuka wakati anafika tu Yanga nilimuambia kuwa ni mchezaji mzuri ambaye atafanikiwa kutokana na jitihada zake.”

Naye Feisal amesema kuwa kama Haruna Niyonzima atapenda kumkabidhi jezi 8 yeye ili aweze kuitumia yeye yupo tayari kutokana na mazuri ambayo ameyafanya Niyonzima ndani ya Yanga akiwa na namba hiyo.

 “Kama Niyonzima atanikabidhi na ataridhia mimi kuvaa jezi namba 8 basi nitakuwa tayari kuivaa jezi hiyo, unajua Niyonzima amefanya mambo makubwa akiwa na namba 8 ndani ya Yanga hivyo ni jezi ya heshima na baraka pia.”


2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic