July 30, 2021


 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji,'Mo' leo Julai 30 amekabidhi mfano wa hudni yenye thamani ya Bilioni 20.

Mkwanja huo ni kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa mabadiliko ndani ya Simba ambao unaendelea na ulikuwa kwenye hatua za mwisho za kuukamilisha mchakato huo.

Mo ameweka wazi kuwa amekuwa akishirikiana na viongozi wa Simba pamoja na mashabiki katika kutafuta mafanikio ambapo timu hiyo imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo na imetwaa Kombe la Shirikisho mara mbili.

Mbele ya Waandishi wa Habari Mo amesema:-"Leo naweka hiyo Bilioni 20 ya hisa asilimia 49 mbele ya mdhamini wa klabu na mwenyekiti wa klabu.

Pia ameweka wazi kwamba mchakato wa mabadiliko umekamilika baada ya kupata hati kutoka FCC ya kuruhusu kumalizia mchakato.

12 COMMENTS:

  1. Hongera Sana Mo,Moja ya mtu mkweli na muaminifu akiahidi basi hutimiza kile alichikiahidi. Ila mtu mwenye roho huishi na roho mbaya hata hili la Mo kutimiza ahadi Kuna watakaobeza na kupandikiza fake news ila kwakweli Simba wapo vizuri Sana Mungu azidi kuwaongoza kwenye mafanikio.

    ReplyDelete
  2. Baada ya masemango sana mataga Leo kaweka vitu adharani inatisha et kimya kimya wakt mchakato ulianza kwa makelele ,

    ReplyDelete
  3. Wajinga ndio waliwao....baada ya kukusanya hela ya wana Simba wenyewe kutoka CAF na kupitia mauzo ya jezi na bidhaa nyingine zenye nembo y Simba anaitumia hiyo hiyo kujifanya anaingiza kwenye klabu kumbe ni kutokana na hela ambayo alikuwa anakusanya kwenye mauzo ya vitu mbalimbali vyenye nembo ya Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wivu huo utopolo mlichonga sana amewafunga midomo

      Delete
    2. Utopolo wivu ndo unawasumbua,kisha wafunga midomo

      Delete
    3. Mo keshawafunika kwenye karai mmebaki hamna ufahamu hata kidogo

      Delete
    4. sawa, ni karai kama lile lile la GSM, au wakati ule Manji, alivyowafunika nyie! kweli nyani haoni kundule!!

      Delete
    5. Utupolo wanateseka sana, wivu umewajaa wanatamani kuona Mnyama anafeli lkn ndo kwanza anazidi kusonga.... Masipobadilika mtazidi kudidimia, msimubujao Mnyama akinyanyua kwapa tena inakuwa mi 5 kuanzia hapo kaulimbiu itakuwa "SIMBAA MITANO TENA"
      mpaka ifike 10

      Delete
  4. Hongera sana Mohamed kwa kufanikisha hlo mana nilihis ni janja janja 2

    ReplyDelete
  5. Vyupi fc mbna hyo kawaida kila tim ipambane na hali yake

    ReplyDelete
  6. Vipi mfano Mo awaahidi Simba msimu huu lazima Simba ichukue ubingwa na isipochukua aulizwe yeye halafu simba isichukue ubingwa hali ingekuwaje? Simba back to back ubingwa wa ligi mara nne. Kuingia robo fainali ya CAF ndani ya miaka mitatu,kombe FA Mara mbili mfululizo, Simba hiyo umekuwa gumzo barani Africa, Sasa jamani wasioitakia mema simba kwanini wasipandikize maneno ya uongo na chuki zidi ya Mo. Uzuri ni kwamba wanasimba sio wapumbavu na Mo mwenyewe ni mwanasimba anaipenda klabu yake kwa dhati kumtenganisha Mo na simba sio kazi rahisi simba imo kwenye Damu yake.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic