July 30, 2021

 


KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, chini ya miaka 23 amesema kuwa amefurahishwa na vijana wake kuweza kutwaa taji la Cecafa 2021.


Ni kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Burundi ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa Uwanja wa Bahir Dar uliopo nchini Ethiopia.

Ushindi wa Tanzania umepatikana kwa penalti 6-5 dhidi ya Burundi baada ya dakika 90 ngoma kuwa nzito kwa timu zote mbili kupata ushindi.

Ni penalti ya mwisho ya kijana Rajab Athuman ambaye alipiga kiufundi ikazama mazima nyavuni baada ya ile ya Akizimana wa Burundi kugonga mwamba mbele ya kipa namba moja Metacha Mnata.

Mnata hakuwa na chaguo leo kwa kuwa penalti zote tano zilizama nyavuni licha ya dakika 90 kutimiza majukumu yake kwa kuokoa michomo mitatu mikali iliyopigwa na washambuliaji wa Burundi.

Poulsen amesema:"Ni furaha kwangu na vijana pamoja na taifa kiujumla kwa kupata matokeo mazuri ambayo tulikuwa tunahitaji.

"Ilibidi nifanye mabadiliko kwenye kikosi kwa sababu wachezaji walikuwa wamechoka kutokana na kucheza mechi nyingi za ushindani ila mwisho wa siku tumeshinda," .

Rais wa TFF Wallace Karia amesema kuwa ni jambo la furaha kwa Tanzania kuweza kutwaa ubingwa huo hivyo bado kazi inaendelea.


Alikuwepo pia makamu wa Kwanza wa Rais Athuman Nyamlani nchini Ethiopia ambapo walishuhidia Tanzania ikitwaa taji la Cecafa.

 

5 COMMENTS:

  1. Kumbe duka alikua mlangoni leo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahahahahahahahahah!!!!!! mpokea ushuru!!!!

      Delete
  2. Ni U-23, ila kanuni ziliruhusu kuwa na wachezaji watatu waliozidi umri huo, yaani "over-aged" players. Kanuni hii hata kwy soka michezo ya Olympics huwa inatumika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic