July 17, 2021

 


ARSENAL mara mbili leo wametoka nyuma na kupata matokeo ya sare ya mabao mawili dhidi ya mawili dhidi ya mabingwa wa Scotland Rangers, katika mchezo wa maandalizi ya msimu.

Ulikuwa ni usajili wa majira ya kiangazi wa Nuno Tavares ambaye aliwarudisha mchezoni Arsenal baada ya bao la kuongoza lililofungwa kwa kichwa na Leon Balogun kwenye kipindi cha kwanza. Cedric Itten aliwatanguliza tena wenyeji hao kwa bao la mpira wa kutenga ambalo baadaye lilisawazishwa na, Eddie Nketiah na matokeo kuisha kwa sare.

Arsenal walionekana kudhamiria kusahihisha makosa waliyoyafanya kweenye mchezo wao wa kwanza, ambao walikubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Hibernian. Kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta ameonekana kuridhishwa sana na kiwango walichokionyesha Arsenal leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic