July 16, 2021

UONGOZI wa kikosi cha klabu ya Azam umekana kuwa kwenye mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Zanaco kutokea Zambia, ambaye pia anawaniwa kwa ukaribu na Simba, Moses Phiri.

Simba wameripotiwa kuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na Phiri, kwa nia ya kumsajili nyota huyo aliyeibuka kinara wa ufungaji bora msimu uliopita.

Azam mpaka sasa imekamilisha usajili wa nyota wawili na kuwatangaza rasmi ambao ni Charles Zulu kutokea Cape Town City ya Afrika Kusini, na beki wa kushoto wa kikosi cha klabu ya Ruvu Shooting, Edward Charles Manyama.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara 2013/14, wanatajwa kumalizana na baadhi ya nyota wa kimataifa ambao ni nahodha wa Gor Mahia ya Kenya, Kenneth Muguna na Paul Katema ambaye klabu yake ya Red Arrows imeonekana kuingilia kati usajili huo kwa madai kuwa hawakumalizana na Azam kwenye dau la usajili.

Akizungumzia ishu ya usajili wa klabu hiyo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Ni weli tumekuwa tukihusishwa na wachezaji wengi katika kipindi hiki cha usajili, na hii mara nyingi inatokana na mahitaji ya wachezaji husika kuongeza thamani zao, hivyo kuhusiana na Moses Phiri na wengine ambao hatujawatangaza hizo zinaendelea kubaki kama tetesi.

“Mpaka sasa wachezaji rasmi ambao tayari tumekamilisha usajili wao na kuwatangaza ni Edward Manyama na Charles Zulu pekee.”

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic