HATIMAYE Kamati ya Usajili ya Yanga,
inayoongozwa na Makamu Mwenyeikiti wake,
Eng. Hersi Said, imedaiwa kufanikiwa
kupenyeza ofa yao ya kumnasa kiungo
mshambuliaji wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini,
raia wa Kenya, Anthon Akumu ili aje kurithi
mikoba ya Haruna Nyinzima.
Tangu Julai 15, mwaka huu, baada ya Yanga
kumuaga rasmi nyota Niyonzima ambaye ni raia
wa Rwanda, imefahamika wazi kuingia moja
kwa moja kwenye mawindo ya kupata mbadala
wake, ambapo imegota kwa Athon Akumu,
anayeitumikia Kaizer.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa timu
ya Kaizer Chiefs, Vina Maphosa, ameliambia
Championi Ijumaa kwamba, ni kweli amesikia
taarifa za Yanga kuleta ombi wakati yeye na
timu hiyo walikuwa nchini Morocco ambako
walienda kwa ajili ya Fainali ya Kombe la
Mabingwa Afrika.
“Kuhusu suala la Yanga kumhitaji Akumu, kwa
sasa mimi siwezi sana kulielezea maana ndiyo
nimetua muda si mrefu nikitokea Morocco,
ambapo nilienda kwa ajili ya mchezo wetu na Al
Ahly, hivyo nitakuwa na mapumziko kwa
takriban siku tano.
“Zaidi nikuombe uwe mvumilivu maana nitajua
hilo suala baada ya kuingia kazini kuanzia
Jumatatu ya Julai 26, mwaka huu, hapo sasa
nitakuwa na majibu ya wazi juu ya jambo hilo,”
alisema Maphosa.
Labda kama mkataba wake umeisha
ReplyDelete