July 25, 2021

 


UWANJA wa Lake Tanganyika,  Kigoma katika fainali ya Kombe la Shirikisho, Simba imetwaa taji Lake mara mbili mfululizo baada ya msimu uliopita kufanya hivyo mbele ya Namungo FC ba leo ilikuwa mbele ya Yanga.


Ni Taddeo Lwanga alipachika bao la ushindi kipindi cha pili ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Ilikuwa ni pigo la kichwa akitumia mpira wa kona iliyopigwa na Luis Miquissone ambaye leo ilikuwa ni kumbukizi yake ya kuletwa duniani.


Ni dakika ya 79 baada ya ngoma kuwa nzito dk 45 za mwanzo ambazo Yanga iliziyeyusha ikiwa pungufu ndani ya uwanja.


Ni Mukoko Tonombe raia wa Congo alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumpiga kiwiko nahodha wa Simba John Bocco ilikuwa dk ya 43.


Simba inatangazwa kuwa bingwa wa Kombe la Shirikisho mbele ya mtani wake wa jadi, mwisho wa reli Kigoma.

37 COMMENTS:

  1. WANYANCHI hoi. Walitafuta kila njia ya mkato hawakufanikiwa. Refa hamna. Manara ilishindikanA. Uchawi wa mzee mpili bure. Vitisho havikufua dafu. Walizidiwa wakabaki faulo baada faulo. Kama simba wangekuea makini hadi 10 wangepigwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Refa mmoja achezeshe mechi nne za timu moja mfululizo uliona wapi Duniani. Alimwambia Bocco agalegale ili apate sababu ya kutoa Red Card. Mikia bila kumnunue mchezaji au refa hamwezi kushinda kombe lolote

      Delete
    2. Mbona husemi timu moja inanyimwa penati mechi mbili mfululizo... Akili zenu hizo ndo zinafanya mshindwe kutengeneza timu mkiamini Simba inashinda kwa kubebwa, mtasubir sana msipo badilika

      Delete
  2. Sasa yanga rasmi inabebwa na simba kimataifa, vinginevyo wasuse hiyo nafasi iliyoletwa na simba. Wakati mwingine waqe wanashukuru tuu.

    ReplyDelete
  3. Chali penelti imeota mbawa. Tumezoea katika sherehe hizi Bwana Manara yuko mbele. Walijigamba kombe ni lao wakaishia nyuso chini na advance ya mabilioni imeshaliwa twamtafuta ndugu Manji hatumuoni. Mungu ni mkubwa

    ReplyDelete
  4. Hatusaidiwi na Simba lakinu kwa juhudi zetu wenyewe. Hahahaaaa. Unachezea mikia

    ReplyDelete
  5. Mungu mkubwa na anapaswa kushukuriwa kwa mapana yasio na kikomo. Simba tumeshinda na ubingwa wa FA tumechukua licha ya figisu tele zisizokuwa za kimpira. Shukrani nyingi ziwaendee wanasimba wote kwa mshikamano waliouneesha mwanzo mwisho wa fainali hii.shukrani pia ziwaendee viongozi na Wachezaji wa Simba na benchi lao la ufundi. Shukrani za kipekee zimuendee Barbara CEO huyu wa Simba. Hakika amepasi moja ya mtihani wake mgumu kabisa tangu kushika wadhifa wake wa CEO.Barbara aliona kuna kitu hakiko sawa kila kunapoelekea Dabi ya simba na Yanga na ujasiri wake wa kumkabili Manara bila ya uoga kwenye suala la kuvujisha Siri za Simba matunda yake tumeyaona leo. Yawezekana Manara alikuwa akitumika kuihujumu Simba bila yeye mwenyewe kujua kuwa alikuwa akitumika na marafiki zake hao viongozi wa Yanga,kosa lake Manara alipokuwa akipewa tahadhari kwake yeye alichukulia nongwa na kuleta uswahili. Hakika kutokuwepo Manara kwenye jopo la timu mipango ya Simba kuliwanyima fursa Yanga kuiba game plan ya Simba na kuwafanya Yanga kucheza Kama timu ya Ndondo pale Lake Tanganyika. Kuna kitu tunatakiwa kujifunza hapa kwamba kweli ni ugumu wa Dabi ndio uliokuwa ukiifanya Simba imara kushindwa kupata matokeo mazuri zidi ya Yanga Dhaifu au kulikuwa na Hujuma?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ikiwa ndivyo hivyo imekuwaje Simba haijashinda goli nyingi kama ilivyoifunga Namungo? Kwanini timu imara ililie penati badala ya kufunga kama ilivyoifunga Namungo kama mashabiki wengi walivyokuwa wakiamini? Je Boko amecheza kiungwana sana mechi ile ya ligi na hii ya kombe ya ASFC? Mnamkosea sana Haji Manara kweli hamna shukrani maana hizo hamasa zake ndio zimewafanya muijue simba

      Delete
    2. Kigego acha pumba

      Delete
  6. Kwa hoyo unajisahaulisha kuwa hizo nafasi kaketa simba wakati mlikuwa bize kuohujumu na vita mara kaizer, acheni hizo.

    ReplyDelete
  7. Leo kombe angebeba yanga,,, hadithi ingekuwa ndefu ya kusoma dakika 20,, ila simba kabeba ndoo ht dakk 1 haifiki habari ishaisha! Haaa haaa

    ReplyDelete
  8. Hakika Yanga wanatia huruma kweli kweli. Yaani ni bora wangefungwa ile mechi ya July 3 kuliko mechi ya leo ambayo kulikua na kombe uwanjani. Wakiambiwa Simba ni wa kimataifa wanajifanya hawasikii

    ReplyDelete
  9. Nimeamini Simba baba lao,Simba oyeeeeeeeeee.Utopolo kimyaaaaaaaa

    ReplyDelete
  10. Mikia aka paka mweusi mpaka mubebwe na refa kwa kutupunguza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bahati mbaya sana tangu filimbi ya kwanza Yanga walionekana wamekuja kucheza mchezo wa judo na si mpira

      Delete
    2. Waliambiwa Simba ukiwachezea vurugu wanashindwa kucheza vizur

      Delete
  11. Hili nalo limepita, tuangalie mbele ya safari

    ReplyDelete
  12. Mikia meshakuwa virobaaa

    ReplyDelete
  13. Leo Matopolo wamelala mapema kama kuku na nguo zao walizonunuwa kusherehekea kombe

    ReplyDelete
  14. Yukowapi Mzee Mpili na Manara wake leo wapewe pole wangoje msimu mpya ambapo wamesajili zaidi ya wachezaji 40 wa kigeni. <

    ReplyDelete
  15. Replies
    1. Refa angekua upande wetu mngekufa zaidi ya bao moja

      Delete
  16. Leo kabla ya kupewa kadi nyekundu Tanombi, wachezaji wa yanga walikuwa tayari wameshaanza kuchoka

    ReplyDelete
  17. Pamoja na Mukoko Tonombe kulalamika kwa refa kuhusu vitendo alivyokuwa anafanyiwa na Bocco lakini refa hakujali ili kumtoa mchezoni Mukoko na kwa hilo walifanikiwa maana ndo lilikuwa lengo la refa na timu yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pumba hzi,mukoko alivyomkanyaga boko tumboni hukuona

      Delete
  18. Fei Toto alisema Simba wepesi, nadhani leo amejifunza

    ReplyDelete
  19. UTOPOLO UTOPOLO UTOPOLO hata hivyo leo imekuwa tu bahati yenu lkn ilikuwa mpigwe nyingi. Refa kapeta penati ya wazi

    ReplyDelete
  20. Yote kwa yote leo imedhihirika ni nani alifuata kucheza kandanda na aliefuata dagaa Kigoma

    ReplyDelete
  21. Fei toto nilisema anaongea ovyo ocyo, sasa leo kacheza nini

    ReplyDelete
  22. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  23. Mnyama kimya na shuari lakini wangeshinda matopolo, kejeli na matusi yangeliendelea kama vile waliposhinda kwa goli moja na ndio mana hawakupata ushindi na kwa sasa kelele zao zimezimika wala hawatotaja tena wajiweke tayari kwa msimu ujao. Hakika Mungu ni mkubwa na Muwweza

    ReplyDelete
  24. Wameshindwa kufumuwa mshoni kama walivoahidi na. kumuandama refa kwa maendeleo na walibaki kujiinamia kamw vile vikongwe vinavochelewa kutuwa kwa ungo

    ReplyDelete
  25. Nyuso zao zilivimba zikawa kama mabunju. Hawaezi kubeba mazito na magazeti ndio yaliyokuwa yakiwazuzuwa hsta wskajiona hapana kama wso wakitoa amri za kupinga kila kitu wakahisi wanaogopwa. Morali imeshatoweka baada ya kujijuwa hawana lolote. Walikuwa wakidema Mnyama wausahau ubingwa sasa wao ndio wasahau. Waliamuni kwa dhati sakata la Manara limeshaivurug Simba na ndipo azima iilipopanda zaidi kwa Mnyama.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic