July 3, 2021


 KIKOSI cha Yanga, leo kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Mchezo wa leo ambapo Simba ilikuwa inahitaji pointi tatu ili kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara mambo yalikuwa magumu kwa timu hiyo iliyoshuhudia pointi tatu zikienda Yanga.

Ni Zawadi Mauya ambaye alikuwa shujaa wa mchezo wa jana kwa kupachika bao moja mbele ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu na kuwafanya Simba wasiamini wanachokiona.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 70 ikiwa nafasi ya pili huku Simba ikibakiwa na pointi 73 baada ya kucheza jumla ya mechi 30.

10 COMMENTS:

  1. Manara waandishi wakimpigia atakuwa mwehu

    ReplyDelete
  2. Ndio Tabu ya kwenda na matokeo mfukoni, poleni watani

    ReplyDelete
  3. Tumeshinda ingawa Simba walijitahidi kipindi cha pili. Kazi safi Yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga ijitahidi katika mechi mbili zilizobaki washinde huku wakiiombea Simba ipoteze zote 4 zilizobaki. Hakuna ajabu yo yote hapo

      Delete
  4. Tumewalaani,wanapoteza zote hao.

    ReplyDelete
  5. Kumpiga mtani raha yake zaidi ya kuchukua kombe,
    Hata wao lenho lao ilikua kuwapiga Yanga ilikuwatambia kibao kimegeuka

    ReplyDelete
  6. Siwaoni wale waliokuwa wanatukana kuhusu yanga au hawajatoka uwanjani hadi sasa

    ReplyDelete
  7. Hakuna furaha kama furaha ya ubingwa kwahivo kamilisha furaha kwa kuuchukuwa ubingwa sio bao moja la nusuranusura

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic