July 13, 2021


 IMEELEZWA kuwa beki wa kikosi cha Azam FC, Yakub Mohamed raia wa Ghana yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Yakub amekuwa hana nafasi kubwa msimu huu kuanza kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba ndani ya Azam FC jambo ambalo linatoa nafasi kwake kuweza kusepa ndani ya Azam FC.

Ugumu unakuja kwenye mkwanja ambao Yanga wanatakiwa kuutoa ili kupata saini ya beki huyo raia wa Ghana kwani bado ana mkataba na matajiri hao jambo ambalo inaelezwa kuwa linawapasua kichwa mabosi wa Yanga.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit aliweka wazi kuwa hakuna mchezaji ambaye wanaweza kumuachia ikiwa wanamuhitaji kwa kuwa hakuna timu yenye uwezo wa kuitikisa timu hiyo.

Kuhusu usajili ndani ya Yanga, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa hawajaanza usajili hivyo yanayosemwa ni tetesi pekee.

"Yanga hatujaanza usajili hivyo hayo yote yanayosikika ni tetesi tu hakuna ukweli katika masuala ya usajili," amesema.

10 COMMENTS:

  1. Yani anayekosa nafasi kwenye kikos kisicho hata na uhakika wa kushika nafasi pili ndo anatakiwa na timu inayojipanga kutafuta ubingwa mwakani na kufanya vizur kimataifa..... Utopolo mtasubir sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Waache uto hao walichokalia ni kutupiga sisi kwenye mshono tu. Sijui wanapata faida gani

      Delete
  2. Kwahiyo Mikia kumsajili Israel KWENDA NI UJINGA?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Israel Mwenda hajakosa namba kwenye timu yake, hujasoma vizuri, rudia

      Delete
  3. Yanga uongo wanauanza wenyewe eti kwa nia ya saikolojiya ya kuishusha morali Simba baadae wenyewe hukanusha

    ReplyDelete
  4. Kwa hesabu zangu mashalla yanga wachezaji wa kigeni wameshafika karibu 30

    ReplyDelete
  5. Mikia acheni kufuata kila kinachoandikwa na waandishi kama bendera inavyofuata upepo. Wanajua mihemko yenu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani kila wakisia yanga wanasajili mchezaji fulani basi ugonjwa wa moyo unawapata, ngoja sasa wasikie manula, chama wamesaini yanga.

      Delete
    2. Nyie wasajilini tu lkn msije mkaanza kulalamika ooh tuna wachezaji maduka.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic