July 23, 2021

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa unahitaji kutwaa taji la Kombe la Shirikisho lililo mikononi mwa Simba hivyo watapambana kupata matokeo chanya.


Tayari timu zote mbili, Yanga na Simba kwa sasa zipo mwisho wa reli Kigoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Julai 25.


Ni katika Uwanja wa Lake Tanganyika,  Kigoma na mwamuzi wa kati atakuwa Ahmed Arajiga ambaye alichezesha robo fainali kati ya Simba v Dodoma Jiji pamoja na nusu fainali kati ya Simba v Azam FC.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema kuwa wanawaheshimi wapinzani wao ila hamna namna nao wanahitaji taji hilo.


"Wapinzani wetu Simba tunawaheshimu lakini hakuna namna kikubwa tunahitaji kushinda ili kupata taji hili muhimu. Mashabiki wajitoleze kwa wingi kutupa sapoti. 


"Ushindi wetu mchezo uliopita wa ligi umetupa nguvu hivyo bado imani ipo na tuna uhakika wa kufanya vizuri,".


Kwenye mchezo wa ligi, Julai 3, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga jambo linaloongeza ushindani katika mchezo huo.

4 COMMENTS:

  1. Hawana Imani na mwamuzi kwa sababu amechezesha mechi nyingi za watani.... Sababu waliyotoa hata ukimueleza mtoto wa darasa la saba mwenye uelewa mzuri wa michezo atashangaa

    ReplyDelete
  2. Hakuna timu hapo ni ubabaishaji tu

    ReplyDelete
  3. Hahahahahaaa mikia bhana wakipigwa utawasikia tumelogwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic