DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga, Julai 25.
Simba wakiwa ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho wanatarajiwa kumenyana na Yanga, Uwanja wa Lake Tanganyika.
Ni majira ya saa 10:00 jioni mbungi hiyo yenye ushindani mkubwa inatarajiwa kupigwa huku tayari timu zote mbili zikiwa zimeshatia timu mwisho wa reli Kigoma.
Gomes amesema:"Wachezaji wapo tayari na wanatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ambao unahitaji matokeo, katika hilo ninaamini wanalijua.
"Tumekuwa na muda mzuri baada ya kukamilisha lengo la kutwaa taji la ligi sasa kazi imebaki hapa kwenye hili la Shirikisho na hakuna njia ambayo tunaweza fanya zaidi ya kushinda.
"Najua kwamba Yanga nao wapo imara wanahitaji kushinda lakini kwa upande wangu nasema tuliweka wazi kuwa tunahitaji kombe hili tutafanya vizuri, mashabiki watupe sapoti,".
Sisi tulimkataa refa ili tupewe wa chaguo letu lakini hatujasikilizwa na biongozi
ReplyDeleteHiyo lugha gani vile?
DeleteKwanini uipangie bodi ya ligi taratibu zakuendesha ligi?yanga mna tabu sana na hakuna wakuwafanya lolote,tunaomba ufike wakati muone japo haya mnafanya mambo kana kwamba nyinyi ndio kila kitu hapa Tanzania kweli inawezekanaje mumkatae refa kwa kigezo eti amechezesha mechi nyingi za watani wa jadi.kwanza mlipaswa kumshukuru kwa alichokifanya siku ile ya dabi ila kwasababu hamkumpa stahiki zake baada ya mechi sasa mnahisi atawalipizia kisasi kwakuchezesha fair game,poleni sasa sisi tunayajua mengi sana mchezo mzima ulivyofanyika tunafahamu kila kitu ila acha muvi iendelee.
DeleteWazee wa pira refa, liliwalipa mechi Ile Ila hii ijayo tusubir tuone
ReplyDelete