August 9, 2021

 


RASMI: UONGOZI wa Yanga leo Agosti 9 umemtangaza nyota mpya Khalid Aucho, winga kutoka nchini Uganda.


Nyota huyo alishuka Tanzania usiku wa kuamkia leo kisha akamalizana na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu,  Nasreddine Nabi. 


Ni miaka miwili amesaini kwa ajili ya kuitumikia timu ya Wananchi ambayo inashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Ligi ya Mabingwa Afrika ni michuano ya kimataifa ambayo Yanga itashiriki baada ya Tanzania kupata nafasi nne za kupeleka timu na timu hiyo ilimaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye ligi.


Aucho amesema:"Malengo ya kila mchezaji ni kucheza timu kubwa, Yanga ni timu kubwa hivyo kwa sasa mimi ni njano na kijani," .

8 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Hapa Simba imeboa kwa kushindwa kumsajili Aucho hasara yake watakuja kuiona muda sio mrefu sijui viongozi wanafikiria nini wanaposema wanaimarisha kikosi?

      Delete
    2. Viongozi wapo busy kuangalia Haji Manara anapost na kusema nini kwenye mitandao

      Delete
  2. Nilidhan kiungo wa kukaba kumbe ni winga

    ReplyDelete
  3. Mbona miaka yote yenu tu hata iliyopita pia

    ReplyDelete
  4. Tutazoa kila kombe lilioko mbele yetu kwa miaka mfululizo tena wakitaka wasitake tusahau maumivu ya miaka mine ta maonevu

    ReplyDelete
  5. Simba kwani hamjui mwenye hela zake anataka kusepa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic