CHELSEA ipo kwenye mazungumzo na Klabu ya Inter Milan ili kuweza kumpata mshambuliaji wao wa zamani Romelu Lukaku ambaye alicheza hapo msimu wa 2011/14 ili aweze kujiunga nao ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22 ndani ya Ligi Kuu England.
Kwa sasa Lukaku mwenye umri wa miaka 28 yupo zake ndani ya Inter Milan ambapo aliibuka hapo akitokea Klabu ya Manchester United. Hivyo mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao ni Chelsea wanahitaji kumchomoa kutoka kwenye kikosi cha Inter Milan ambacho kinashiriki Serie A.
Msimu huu ndani ya Serie A nyota huyo amefunga jumla ya mabao 24 pasi 11 za mabao na mashuti jumla ya 48 ambayo yalilenga lango.
Ofa ambayo imewekwa mezani ni pauni milioni 85 na Chelsea wapo tayari kutoa mchezaji mmoja ambaye atafanya dili liwe jepesi. Lukaku mwenyewe amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya kikosi hicho cha Inter Milan ya Italia ambao wametwaa ubingwa msimu uliomeguka baada ya kuyeyuka miaka 1.
Chelsea wamebaki kuwa na chaguo la kumpa saini Lukaku ambaye anasema hajafikiria kuondoka kwa sasa na akili zake ameziweka kwa ajili ya msimu mpya. Licha ya kwamba Inter Milan wenyewe hawapo tayari kumuachia nyota huyo raia wa Ubelgiji imani ya Chelsea ipo katika kumpata nyota huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment