IMEELEZWA kuwa mabosi wote wawili wa Simba na Yanga walikuwa kwenye presha kutokana na ishu za kukamilisha sajili kwa wachezaji wao wawili ambao tayari wameshamwaga wino.
Ilikuwa ni kwa Simba juu ya mchezaji wao winga Peter Banda ambaye amesaini dili la miaka mitatu kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.
Nyota huyo mwenye miaka 20 hivi karibuni iliripotiwa kwamba Yanga wamemdaka juu kwa juu na kumalizana naye na ilitarajiwa kutambulishwa hivi karibuni.
Jana Agosti 3 alitambulishwa Banda ndani ya Simba na kuzima zile presha ambazo zilikuwa zipo kwa mashabiki pamoja na viongozi.
Kuhusu hilo Yanga waliweka wazi kwamba wao hawakuwa na mpango wa Banda hivyo yote yaliyokuwa yakielezwa ilikuwa ni tetesi.
Kwa upande wa Yanga ambao jana walimtambulisha Makambo kwa dili la miaka miwili kabla ya kutambulishwa rasmi inaelezwa kuwa simu yake ilikuwa haipatikani.
"Simu ya Makambo ilikuwa haipatikani muda mfupi kabla ya kutambulishwa, sasa jambo hilo lilimfanya presha iwe kubwa na mwisho wa siku wakampata.
"Kumbe ilikuwa simu imeisha chaji na Makambo aliendelea na mambo yake mpaka alipopatikana hali haikuwa shwari," ilieleza taarifa hiyo.
Tayari kwa sasa Makambo ni mali ya Yanga na Banda ni mali ya Simba.
Utopolo munajitekenya wenyewe na mnacheka wenyewe kaz, kwenu banda huyooooooh! kamwaga wino.
ReplyDeleteSasa kumbe presha ilikuwa kwenu Yanga mkaihusisha Simba ya nini? Ama kweli hili dili la usajili mpaka limalizike tutasikia mengi.
ReplyDeleteNi utoto tuu. Halafu siku nyingine mkisajili tumieni official platform na nembo za wafadhili wenu zionekane background. Sio mnasajili sebuleni kwa mtu, ushauri tuu.
ReplyDeletePresha ya yanga no ya kujitakia, hivi kweli makambo ni wa kutakiwa na Simba yenye Boko, Mugalu na Kagere?
ReplyDeleteNyie mikia endeleeni kucheza twist na madalali.
ReplyDelete