August 3, 2021


NYOTA wa Biashara United, Daniel Mgore kwa sasa yupo huru kujiunga na timu yoyote baada ya dili lake kumeguka ndani ya timu hiyo.

Biashara United ina uhakika wa kushiriki mashindano ya kimataifa ambapo itakuwa katika Kombe la Shirikisho na inakuwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo.

Ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya nne na ilikusanya jumla ya pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 34 na Mgore alikuwa ni kipa namba moja wa timu hiyo.

Sababu ya kupenya kimataifa ni Tanzania kuwa na nafasi nne za uwakilishi kimataifa baada ya kufikisha vigezo vya kuwa na pointi nyingi ambazo zilichangiwa na Yanga pamoja na Simba ambao waliwahi kutinga hatua ya robo fainali ila kwa msimu hii ni Simba iliweza kufanya vizuri kimataifa kwa kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Uwezo wake ulikuwa imara ambapo ndani ya msimu wa 2020/21 alikusanya jumla ya clean sheet 11 ikiwa ni pungufu ya zile 6 kwa kuwa msimu uliopita alikusanya clean sheet 17 ndani ya Biashara United.

Kipa huyo amesema:"Mkataba wangu uliiisha pale msimu ulipoisha hivyo kwa sasa nipo huru kujiunga na timu yoyote ila kipaumbele kikubwa ni hapa nilipo," .

3 COMMENTS:

  1. Mwandishi acha kuwadangaya yanga, point zinazowapeleka biashara na hao yanga kucheza michezo ya CAF zimechangiwa na simba, yanga kachangia nini sasa.

    ReplyDelete
  2. Pointi nyingi ambazo zilichangiwa na yanga pamoja na Simba ..... Wacha weeeee

    ReplyDelete
  3. Yanga kachangia point kwa vipi, ana miaka hajakanyaga hata makundi tuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic