NYOTA 8 ndani ya kikosi cha Yanga hawana uhakika wa kubaki ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao wa 2021/22 kutokana na rekodi kuwakataa mazima.
Tayari wawili wameshajua hatma yao ambao ni Haruna Niyonzima ambaye aliagwa kwenye mchezo dhidi ya Ihefu pamoja na beki Lamine Moro ambaye huyu walikubaliana kuvunja mkataba wake.
Kwa mujibu wa rekodi za Championi Jumatatu ni nyota 8 ambao hawakuwa na mwendo mzuri katika kikosi cha kwanza na mchango wao ulionekana ni mdogo jambo ambalo linawafanya wasubiri hatma yao na neno kutoka kwa Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Rekodi zinaonyesha kuwa Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 34 ni mechi 8 Wazir Junior aliweza kucheza na alifunga mabao mawili licha ya kwamba ni mshambuliaji kati ya mabao 52. Na alikwama kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita alipokuwa Mbao FC ambapo alifunga mabao 13.
Ditram Nchimbi alitupia bao moja kwenye mechi zote 25 alizocheza ilikuwa mbele ya Gwambina FC inaelezwa kuwa anaweza kuibukia Biashara United. Michael Sarpong mwilijumba alicheza mechi 23 na alifunga mabao manne jambo linalowafanya mabosi kufikiria kuvunja mkataba wake.
Mzawa Paul Godfrey yeye ni beki alicheza jumla ya mechi tatu na hana nafasi kikosi cha kwanza kwa zama hizi za Nabi huenda akaachwa ama kutolewa kwa mkopo.
Kipa namba tatu Ramadhan Kabwili alidaka mchezo mmoja kati ya 34 ilikuwa dhidi ya Dodoma Jiji na hakufungwa kwenye mchezo huo kwa kuwa dk 90 ngoma ilikuwa 0-0.
Said Juma Makapu yeye ni beki wa kati alicheza mechi 6 pekee. Fiston Abdulazack ingizo hili jipya kwenye dirisha dogo ni mechi 7 za ligi alizocheza na alifunga bao moja pekee mbele ya Polisi Tanzania na alifunga bao lingine kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho. Hana nafasi ya kudumu na tayari aliweka wazi hivi karibuni kuwa hana hesabu za kubaki ndani ya Yanga.
Kiraka Farid Mussa maisha yake yamekuwa tofauti na vile ambavyo walifikiria na alicheza mechi 19 na alitoa pasi mbili za mabao.
Kuhusu mchakato wa kuacha wachezaji, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli aliliambia Championi Jumatatu kuwa masuala ya usajili yapo kwenye benchi la ufundi.
Kuhusu kuvunja mikataba ya wachezaji, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa huwa kunakuwa na ugumu katika kuvunja mkataba kwa kuwa sio jambo rahisi.
Kwa Mnyama kimyaaaa hakuna mbwenbwe wala msjisifu, sifa yao wakisema wanatenda bila ya papara
ReplyDeleteIli wauze magazeti lazima wawataje wananchi. Mikia mmm..
ReplyDeleteFarid Mussa yuko vizur sidhan Kama anastahili kuachwa
ReplyDeleteWaandishi wajanja wanaangalia mashabiki wapi wepesi kudanganyika, wanagundua ni utopolo
ReplyDeleteWanaodanganywa ni mikia fc ndio maana kikisemwa chochote kuhusu Wananchi lazima watoe comment tena za hovyo. Yanga brand kubwa ndio maana inawapa shida katika kuikabiri kistaarabu. Msemaji pamoja na washabiki wao wanamhaho tena wa kimilenia
ReplyDeleteMoja ya njia ambayo inasaidia kujua kama kweli timu unayoishabikia ni 'brand' kubwa au la Africa, ni kuangalia latest rankings (viwango vya ubora) za CAF. Hapo utaona kuna timu ya Tanzania ni ya 12 kwa ubora, wakati zingine hata rankings zao nì mgogoro!!! Na uzuri ni kwamba rankings hizi hazitengenezwi na Karia!!
ReplyDeleteMsimu ujao hakuna Covid'19 wachezaji wengi katika kila nchi watakuwa wamechanjwa kwa hiyo hakutakuwa na woga
Delete