NYOTA wa timu ya Aston Villa na nahodha pia Jack Grealish amerejra mazoezini kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya mabosi wa Manchester City kukwama kulipa dau la pauni milioni 100 ambazo zilikuwa zinahitajika ili kuipata saini yake.
Grealish ambaye alipewa muda wa mapumziko na timu yake baada ya kushiriki kwenye mashindano ya Euro 2020 akiwa na timu ya taifa ya England alionekana akiwa na wachezaji wenzake kwenye mazoezi Jumatatu.
Nyota huyo mwenye miaka 25 ameonekana kuwa na nidhamu uwanjani na hata msimu uliopita alikuwa kwenye ubora kwa kufanya vizuri jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Manchester City kupiga hesabu kupata saini yake.
City wanamfuatilia kwa ukaribu kiungo huyo na wanahitaji kuipata saini yake kwa msimu huu kwa mujibu wa Sky Sports wanatarajia kupeleka ofa yao siku ya Ijumaa na dau ambalo watapeleka ni pauni 100 ambazo zinahitajika na mabosi.
0 COMMENTS:
Post a Comment