WAKATI huu wa dirisha la usajili likiwa limefunguliwa, benchi la ufundi la Ruvu Shooting lipo sokoni kusaka majembe saba ya kazi kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21.
Kwenye upande wa ulinzi, Ruvu Shooting ambayo ilimaliza msimu wa 2020/21 ikiwa nafasi ya 11 na iliokota jumla ya mabao 38 itakosa huduma ya beki wao Edward Manyama ambaye kwa sasa ni mali ya Azam FC.
Kwa mujibu wa ripoti ya Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa ambayo tayari mabosi wamekabidhiwa inaeleza kuwa inahitaji nyota saba ikiwa ni pamoja na eneo la beki wa kushoto alipokuwa Manyama pamoja na eneo la kipa.
Mkwasa amesema:"Tunahitaji kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu ujao kwa kuhitaji wachezaji bora na mahitaji mengi katika kikosi chetu ukiangalia msimu uliomalizika tulishindwa kufikia malengo ya kumaliza nafasi nne za juu.
"Sababu kubwa ni kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya wachezaji wangu hivyo hatutaki kuona inatokea msimu ujao," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment