August 19, 2021


 TIMU mbili za Ligi Kuu Bara ambazo ni Coastal Union ya Tanga na Mbeya Kwanza ya Mbeya zinapambana kuipata saini ya kipa namba moja wa Mwadui, Mussa Mbissa ili awe ndani ya timu zao.

Mbeya Kwanza imepanda Ligi Kuu Bara msimu uliopita ikitokea Ligi Daraja la Kwanza hivyo itashiriki Ligi Kuu Bara.

Awali ilikuwa inatajwa kuwa kipa huyo angeibukia ndani ya kikosi cha Yanga ila dili lake limebuma baada ya Yanga kupata makipa wapya wawili ikiwa ni pamoja na Erick Johora mzawa aliyeibuka katika kikosi hicho akitokea Aigle Noir ya Burundi.  

Msimu uliopita ndani ya Mwadui FC alikuwa ni kipa namba moja wa timu hiyo licha ya kuwa ni namba moja kwa kufungwa mabao mengi ambayo ni 57 bado alikuwa anaweza kuoka hatari nyingi.

Mbissa amesema kuwa ni kweli ana ofa kibao kwa timu nyingi ambazo zinahitaji ila ataweka wazi pale watakapofikia muafaka mzuri.


“Kweli kuna ofa kutoka timu mbalimbali ambazo zinahitaji huduma yangu ikiwa ni pamoja na Coastal Union na Mbeya Kwanza. Ninachoangalia ni dau yule ambaye atakuwa na dau kubwa nitasaini.


“Sijafanya maamuzi ya wapi nitakuwa lakini haitachukua muda mrefu nitajua wapi nitakuwa hivyo ni suala la kusubiri,”.

7 COMMENTS:

  1. Kwamba kuhtajika na yanga tayari ni kipa wa yanga??

    ReplyDelete
  2. Sometimes matusi mnayakaribisha wenyewe kwa kuandika upuuzi

    ReplyDelete
  3. Akiwa mwadui aliipambania sana yanga hadi kuipatia magoli, anastahili kuitwa kipa wa yanga

    ReplyDelete
  4. Heading na content vitu viwili tofauti kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic