AFRIKA inamtambua nyota huyu, dunia inamtambua anatajwa kwamba huenda ni mchezaji bora wa muda wote kupata kutokea katika bara la Afrika, ndiyo ni bara la Afrika. Alikuwa anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.
Jina lake ni Augustine Azuka hapo naweza nikawa nimekupoteza ila jina lake maarufu ni Jay-Jay Okocha, hapo naaamini tupo pamoja. Nyota huyu ni raia wa Nigeria ana umri wa miaka 48.
Aliletwa duniani Agosti 14,1973 alikuwa ni mchezaji tegemeo katika timu yake ya taifa ya Nigeria. Alianza kucheza tangu ile timu ya watoto jambo lililomfanya kuwa gumzo kila kona kutokana na uwezo wake zama akicheza mpira.
Katika timu ya wakubwa ya taifa ya Nigeria alicheza jumla ya mechi 73 na alifunga mabao 14. Anakumbukwa kwa bao lake la pigo huru Julai 3,1993 mbele ya Algeria katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia na mwisho wa siku timu yake ilishinda kwa mabao 4-1.
Ana tuzo kibao kabatini ikiwa ni pamoja na ile ya bao bora la mwaka 1993, mchezaji bora wa Nigeria alitwaa tuzo 7 ilikuwa mwaka 1995, 1997, 2000, 2002, 2003, 2004, 2005. Pia ni mchezaji aliyekuwa ndani ya kikosi bora cha FIFA cha mastaa wote wa Kombe la Dunia 1998 ila alikuwa mchezaji wa akiba. Mchezaji bora wa mwezi ndani ya Ligi Kuu England Novemba 2003, mchezaji bora wa Afrika 2004 katika Afcon.
Katika timu amecheza jumla ya mechi 454 na alifunga mabao 89. Rekodi zinaonyesha kuwa ni ndani ya Bolton Wanderers alicheza mechi nyingi ambazo ni 124 ilikuwa msimu wa 2002/2006 alijiunga na timu hiyo akitokea PSG ambapo alidumu hapo kuanzia msimu wa 1998/2002.
Tafadhali mwandishi, msimu wa 2002/2006 na msimu wa 1998/2002 ndo nini. Jifunzeni kuandika Kwanza ndo mje mtuandikie sio mnkurupuka tu
ReplyDelete