August 19, 2021


 GEORGE Ambangile, mchambuzi wa masuala ya michezo amesema kuwa wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa, Simba watakutana na ugumu tofauti kwenye mashindano hayo hivyo wanapswa wajipange sawasawa. 


Akizungumza na Saleh Jembe, Ambangile amesema kuwa kutokana na mafanikio ambayo waliyapata Simba kwa kutinga hatua ya robo fainali kutawafanya wapinzani wao waje kwa mfumo tofauti jambo litakalomfanya Kocha Didier Gomes kuwa na kazi ya kufanya.

Ambangile amesema:-"Ukiwa mkubwa haina maana kwamba haufungwi hapana, tumeona kwamba Al Ahly ilifungwa na Simba, Kaizer Chiefs walifungwa na Simba pia Uwanja wa Mkapa hivyo kinachotakiwa ni mbinu na kujua jambo la kufanya.

"Kutinga hatua ya robo fainali kwa Simba ni jambo zuri lakini litawafanya wapinzani wao kujipanga na kuja na mbinu tofauti katika mechi zao zijazo hapo lazima wajipange.

"Imani yangu ni kwamba kocha Gomes anajua namna ya kwenda na vijana wake katika kusaka ushindi hivyo kikubwa ni kusubiri na kuliachia kai benchi la ufundi kuweza kuyatimiza malengo ambayo wamejiwekea," amesema.

Kwa sasa Simba imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 imeanza kazi ikiwa na wachezaji wake wapya iliowapa madili mapya ambao ni pamoja na Duncan Nyoni, Israel Mwenda pia wapo wale waliokuwepo kwa muda mrefu ambao ni Said Ndemla, Jonas Mkude, Pascal Wawa, Meddie Kagere. 


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic