MAISHA yanazidi kuendelea kwa sasa ikiwa ni wakati wa usajili ndani ya ardhi ya Bongo kwa ajili ya msimu wa 2021/22.
Mshtuko kwa mashabiki wa Yanga umekuwa ghafla baada ya makipa wake wote wawili kutemwa mazima jambo linalomaanisha kwamba ni sura mpya zitakuwa langoni msimu mpya.
Makipa hao wawili wapo huru kwa sasa baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi kutokuwa tayari kufanya nao kazi.
Hapa ni rekodi za makipa hao wawili ambao wataanza maisha mapya msimu ujao katika changamoto mpya. Katika mechi 34 ni moja pekee alikaa langoni Ramadhan Kabwili abaye yupo nchini Morocco na kikosi ilikuwa mbele ya Dodoma Jiji:-
Mnata
Metacha Mnata kwa sasa safari yake imewadia akiwa huru kusaini dili jipya timu nyingine baada ya mkataba wake kukamilika.
Ni mechi 23 ambazo alicheza alikuwa ni chaguo namba moja kwa makocha ambao walipita Yanga. Zama za Cedrick Kaze na sasa alimaliza na Nasreddine Nabi ambaye ni muumini mzuri katika suala la nidhamu.
Mnata katika mechi hizo aliyeyusha dakika 2,070 aliruhusu mabao 13 ya kufungwa.
Anatunguliwa kila baada ya dk 159
Kipa huyo mzawa ana wastani wa kuokota nyavuni bao moja kila baada ya dakika 159 katika mechi ambazo amecheza jambo linaloonyesha kwamba uwezo kwenye mikono yake ni mkubwa.
Amekusanya jumla ya clean sheet 13 na alifungwa katika mechi 10 ndani ya ligi msimu wa 2020/21.
Timu ya Yanga ilimaliza msimu ikiwa nafasi ya pili na msimu ujao wa 2021/22 itashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika bila uwepo wa mikono ya nyota huyo.
Hapa alikuwa shujaa
Yanga 1-0 Mbeya City, Kagera Sugar 0-1 Yanga, Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Yanga 3-0 Coastal Union, Yanga 1-0 Polisi Tanzania, Biashara 0-1 Yanga, Gwambina 0-0 Yanga, Azam 0-1 Yanga, Yanga 1-0 JKT Tanzania, Mwadui 0-5 Yanga, Ihefu 0-3 Yanga.
Namungo 0-0 Yanga na JKT Tanzania 0-2 Yanga.
Alionja joto ya jiwe
Tanzania Prisons 1-1 Yanga, Mbeya City 1-1 Yanga, Kagera Sugar 3-3 Yanga, Yanga 3-1 Dodoma Jiji, Yanga 2-1 Ruvu Shooting, Yanga 1-1 Simba, Yanga 1-1 Namungo, KMC 1-2 Yanga, Polisi Tanzania 1-1 Yanga, Ruvu Shooting 2-3 Yanga
Utata ulianzia hapa
Juni 17 aliweka mkataba wake rehani baada ya uongozi wa Yanga uliamua kumsimamisha kwa muda usiojulikana kutokana na kitendo chake kisicho cha kiuungwana kwa mashabiki ambao walikuwa wakimzomea kwa kueleza kwamba alifanya uzembe katika kuokoa bao la pili ambalo lilifungwa na David Richard, dakika ya 82.
Mwisho picha inakamilika kwa Metacha kutuongezewa dili jipya na sasa yupo huru kujiunga na timu itakayomhitaji.
Shikalo
Faroukh Shikalo naye safari imemkuta baada ya dili lake la miaka miwili kumeguka.Alicheza jumla ya mechi 10 ambazo ni dakika 900, alikusanya clean sheet nne na alifungwa katika mechi sita.
Jumla alifungwa mabao 8 akiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 112.
Hapa alitunguliwa
Yanga 1-1 Prisons, Coastal Union 2-1 Yanga ,Yanga 1-1 KMC, Yanga 3-1 Gwambina, Yanga 0-1 Azam FC ,Yanga 3-2 Mwadui.
Hapa alikuwa shujaa
Yanga 1-0 Mtibwa,Yanga 1-0 Biashara United, Simba 0-1 Yanga, Yanga 2-0 Ihefu.
Ndugu mwandishi zingatia na uelewe kwamba kwenye maisha ya ajira za kisasa kunaxingatiwa sana kitu inaitwa A.S.K(Attitudes, Skills n Knowledge). Siyo uwezo tu unaokuhakikishia ajira.
ReplyDeleteRekodi zinaweza kuwa nzuri kama nidhamu ni mbaya utapata taabu sana.
Unapata clean sheet, ni kwa uwezo binafsi au mguvu kubwa na jasho la wengine? Hujaelezea magoli waliyofungwa Metacha na Farouk ni ya aina gani; goli la Dodoma Jiji mechi ya Arusha, goli la Onyango, magoli 2 ya Kagera, goli la Ruvu shooting, goli la Polisi mechi ya Moshi, goli la Steven Sey mechi ya Dar, yangetosha kumfikirisha mwajiri yeyote.
Hata maudhui ya uhariri wako bado yanafikirisha, unalenga kuwatetea, kuwalaumu Yanga au kuwananga makipa Diara na Johora; waliochukua nafasi zao?, manake Kabwili umemponda waziwazi.
Ajira ni zaidi ya sifa wala ujuzi.