August 31, 2021


WAKATI dirisha la usajili Ulaya likitarajiwa kufungwa leo Agosti 31 usiku, Liverpool inatajwa kuwa katika hesabu za kuwa kwenye anga za za kunasa saini za baadhi ya nyota.

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa katika rada hizo ni Saul Niguez ambaye ni kiungo ndani ya Klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya Hispania ana umri wa miaka 26 alikuwa anatajwa kuwaniwa pia na Manchester United.

Yupo pia Renato Sanches kiungo anayecheza ndani ya Ligue 1 akiwa katika Klabu ya Lille na ana umri wa miaka 24 alikuwa anatajwa pia kuwaniwa na Wolves.

Kylian Mbappe mshambuliaji wa PSG huyu Real Madrid wanampigia hesabu kali wanashindana katika dau tu kwa sasa na Adama Traore, mwenye miaka 25 akiwa anacheza winga ndani ya Wolves alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Spurs pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic