KLABU ya Birmigham imethibitisha kukamilisha usajili wa Troy Deeney kwa dili la miaka miwili baada ya mshambuliaji huyo kuyeyusha jumla ya miaka 11 akiwa ndani ya Watford inayoshiriki Ligi Kuu England.
Deeney mwenye miaka 33 amesema kuwa kwa kila jambo ambalo alifanya ndani ya timu hiyo kwake ni furaha hivyo anahitaji kuweza kupata changamoto mpya katika maisha mapya ambayo anakwenda kuayaanza.
Anakwenda kujiunga na timu yake ya utotoni Birmingham inayoshiriki Championship baada ya kukubali dili lake la miaka miwili ambalo litameguka mwaka 2023 ukiwa na kipengele cha kumuongezea dili lingine tena ikiwa ataweza kufanya vizuri.
Mshambuliaji huyo alijiunga na Klabu ya Watford mwaka 2010 akitokea Klabu ya Walsall na aliweza kufunga jumla ya mabao 140 huku lile lililopata umaarudfu ni lile alilowatungua Leicester City 2013 na mabao hayo alifunga kwenye mechi 419 ambazo alicheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment