BEKI mpya wa Simba, Henock Inonga Baka amesema kuwa Chris Mugalu ndiye mchezaji ambaye anampa ushirikiano mkubwa katika kuyazoea kwa haraka maisha yake ndani ya Simba.
Baka ambaye ni beki wa Kati, amesajiliwa na Simba akitokea katika Klabu ya DC Motema Pembe ya nchini DR Congo.
Baka amesema kuwa Mugalu amekuwa akimpa ushirikiano mkubwa wa kuhakikisha kuwa anayazoea mazingira mapya ndani ya Simba pamoja na kumfundisha jinsi ya kuongea Kiswahili.
“Mimi na Mugalu ni marafiki tangia zamani, nimefurahi kumkuta hapa ndani ya Simba yeye ndiye anafundisha kila kitu kuhusu Simba na kuzungumza kiswahili hivyo nashukuru kwa hilo,".
Nyota huyo anatarajiwa kuwa katika maisha mapya ndani ya ardhi ya Tanzania kwa msimu mpya wa 2021/22 akiungana na nyota wengine kama Israel Mwenda pamoja Peter Banda ambao wamesajiliwa na timu hiyo.
Kazi kubwa ni kuweza kutetea mataji ambayo ilitwaa kwa msimu uliopita wa 2020/21 pamoja na kuweza kuweka rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment