August 4, 2021

 


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imekubali ofa ya dola za Marekani 900,000 (zaidi ya Tsh Bilioni 2) kumuuza kiungo mshambuliaji wake Luis Miquissone.

Raia wa Msumbiji aliwapa tabu mabosi wa Klabu ya Al Ahly ya Misri walipokutana nao kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa aliwatungua bao moja akiwa nje ya 18.

Nyota huyo kuna uwekezako mkubwa msimu ujao akwa kwa Waarabu hao wa Misri ambao ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa mara mbili mfululizo.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa tayari Simba na Ahly wamefikia makubaliano hayo ambapo Miquissone amekubali kujiunga na Al Ahly kwa mkataba wa miaka minne.


Kutokana na dili la kiungo huyo mwenye kasi awapo uwanjani huku mguu wake wa kushoto ukiwa ni pendwa kwake tayari Simba wamempa dili la miaka mitatu Peter Banda ambaye anatajwa kuwa mbadala wake.

7 COMMENTS:

  1. Kama taarifa hazijatoka ndani ya Simba basi hizi ni taarifa ni za uongo. Tunajua Miqisone ataondoaka au hata kusalia ndani ya simba ila acheni viherehere mpaka wenyewe Simba watoe kauli rasmi kwani tayari mlashazua uongo wa kutosha kuhusiana na huyo Banda.

    ReplyDelete
  2. Ni Simba tu peke yake ambapo mastaa wake pamoja na hata makocha wake kuwa kivutio kikubwa Africa na kwengine duniani na kutakiwa kwa bei ambazo hazijawahi kutokea hapa nyumbani hivo kuifanya timu iwe maarufu,kupendwa na kuheshimiwa. Haya yanawaumiza wasio na shukuru. Ewe Mungu zidi kukibariki Simba

    ReplyDelete
  3. Tafautisha kusajili wachezaji na wakimbizi ukisajili mchezaji utamuza kwa pesa nyingi na ukisajili wakimbizi utabaki wakukimbie

    ReplyDelete
  4. Kibaya chajitembeza lakini kizuri daima chajiuza wenyewe

    ReplyDelete
  5. Safi sana watani zangu ndivyo inavyotakiwa hivyo, ningeshangaa sana km mngeikataa hiyo ofa hongereni

    ReplyDelete
  6. Banda atakiwasha cha Luis mara mbili. Simba ni chaguo la Mungu linapokuja suala la mashindano ya kimataifa. Hata watani zetu wanalijua hili

    ReplyDelete
  7. Ukubwa wa timu wakutaje watu sio kujisifu mwenyewe mana wapo wanaojisifu wa kihistoria twambieni ipo labda ni timu ya kwanza duniani kununua golikipa kwa pesa nyingi kuliko foaf(kaseja)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic