August 4, 2021


 KIUNGO wa Polisi Tanzania, Hassan Nassoro inaelezwa amemalizana na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kuwatumikia kwa msimu ujao.

Nassoro mwenye rasta kichwani amekuwa na msimu mzuri ndani ya uwanja licha ya jina lake kuwekwa kwenye orodha ya wale waliomaliza mkataba na hawataongeza mkataba.

Mtu wa karibu wa Nassoro amesema kuwa mabosi wa Yanga wamefanya mazungumzo na Nassoro hivyo ni suala la muda kufikia makubaliano ya kusaini dili jipya.

"Nassoro kwa sasa yupo huru kujiunga na timu ambayo itafikia dau la kumpa kandarasi mpya lakini Yanga wameonekana kuwa karibu kumpa mkataba hivyo ni suala la kusubiri," ilieleza taarifa hiyo.

Alipotafutwa Nassoro alisema kuwa bado kwa sasa hajapata taarifa kuhusu kujiunga na Yanga.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga katika Kamati ya Mashindano amesema kuwa mipango ya usajili ipo na wanaamini watafanya mambo hayo kwa umakini.

Tayari Yanga imemsajili Yusuph Athuman, Fiston Mayele na Heritier Makambo na wameweka wazi kwamba kazi inaendelea.



10 COMMENTS:

  1. Ndipo. Tunapofeli sisi Yanga yaani ikifika wakati huu ndio utajua kuwa Uongozi wa Yanga ni dhaifu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bora wewe umegundua ukweli ulipo wengine bado wamelala

      Delete
    2. Lazima wazawa wapewe nafasi

      Delete
    3. Wewe, Hassan Maulid ni kiungo mzuri mno labda kama hujawahi kumuona uwanjani.Ana piga dimba la kati vizuri sana.

      Delete
  2. Bila kuitaja Yanga huwezi pandisha thamani ya mchezaji. Lazima utasikia Yanga ikihusishwa kuliko timu yoyote nyakati hizi

    ReplyDelete
  3. Huyo ni mbadala wa Aucho maana nasikia Mnyama nae kapanda dau

    ReplyDelete
  4. Acheni kuhadaiwa na habari za hawa madalali.Kila mchezaji wanaetaka kumpigia promo lazima waitaje Yanga ili ku create attention

    ReplyDelete
  5. Yanga inaonekana ni gia nzuri madriver watuambie gia gani huwa gari inakuwa nzuri kwani Kila mchezaji gia yeke inaanza na Yanga kwani Nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic