IMEELEZWA kuwa nyota wa Namungo FC, Stephen Sey yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya Yanga.
Yanga ilikuwa kwenye mpango wa kuinasa saini ya nyota huyo msimu huu kwenye dirisha dogo ila mambo yaligoma baada ya kocha Cedric Kaze kumpotezea.
Kwenye ripoti ya Kaze ambaye alichimbishwa mazima inaelezwa kuwa alimtaja Fiston Abdulazack ambaye alipewa dili la miezi sita na limemeguka kwa sasa hajaongezewa dili jingine.
Habari zimeeleza kuwa mabosi wa Yanga wamemfuata tena Sey ili wamuongeze kwenye kikosi raia huyo wa Ghana ambaye alipata nafasi ya kumtungua Metacha Mnata walipokutana Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa ligi uliokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kuhusu usajili Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga alisema kuwa mipango ipo na watasajili kwa umakini.
Aiseee Mwandishi unatisha
ReplyDeleteKifupi unajikaza
ReplyDeleteWann huyo sasa?🤑🤑🤑
ReplyDeleteKila kitu tanga mbona huandiki anaenda simba
ReplyDelete