PETER Banda ameletwa duniani Septemba 22,2000 hivyo kwa sasa ana umri wa miaka 20 raia huyo wa Malawi ambaye anacheza pia timu ya taifa ya Malawi.
Nyota huyo ni mali ya Klabu ya Simba ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa na anatajwa kwamba amejiliwa Simba kuwa mbadala wa kiungo Luis Miquissone.
Luis mwenye mabao 9 na pasi 10 za mabao ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 huenda akaibukia ndani ya Al Ahly ya Misri ambao aliwatungua bao moja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Banda yeye ni winga na uwezo wake ni kwenye miguu yote miwili kulia na ule wa kushoto katika kufanya maamuzi ndani ya uwanja.
Aliibuka ndani ya Simba akitokea Klabu ya Big Bullets ambayo ilimtoa kwa mkopo katika Klabu Sheriff ya Moldovia ambapo huko alipata nafasi ya kucheza jumla ya mechi 15 na alitupia mabao matano.
Mkononi ana tuzo ya mfungaji bora ambapo alitwaa akiwa na timu ya taifa ya Malawi chini ya miaka 17 mwaka 2016 katika mashindano ya Cosafa yaliyofanyika nchini Mauritius.
Alifunga jumla ya mabao matano wakati akitwaa tuzo hiyo na katika hayo mabao alifunga hat trick kwenye hatua ya makundi walipokutana na Kenya katika hatua ya makundi na timu yake ilishinda kwa mabao 5-0. Mfungaji namba mbili alikuwa ni nyota kutoka Nambia ambaye ni Abram Tjahika ambaye alifunga mabao manne.
Kwenye mashindano hayo Malawi iligotea nafasi ya tatu na mabingwa walikuwa ni Namibia baada ya ushindi mbele timu ya taifa ya Afrika Kusini.
Nyota huyo ni mtoto wa zamani wa mchezaji wa timu ya taifa ya Malawi na Big Bullets Chikondi Banda.Nafasi ambayo alikuwa akicheza zama za uhai wake ilikuwa ni kiungo pia.
Rekodi zinaonyesha kwamba Chikondi Banda alitangulia mbele za haki Agosti 8,2013 na aliletwa duniani Desemba 28. 1979.
Hivyo nyota huyo amekuwa akipita kwenye nyayo za baba yake ambaye alikuwa mchezaji na katika timu ya taifa ya Malawi rekodi zinaonyesha kwamba alicheza jumla ya mechi 7 na alitupia bao moja.
Dogo tunakutegemea uje kuziba pengo la kipenzi chetu sio vinginevyo karibu msimbazi
ReplyDeleteKwamba kazaliwa 2000. akaibuka mfungaji bora 2016. wakati huo baba yake alifariki 2013. Shukrani kwa taarifa
ReplyDelete