August 4, 2021


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha wa Makipa, Razack Siwa leo Agosti 4 kimelazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Klabu ya Atlabara.

Ni kwenye mchezo wa Kombe la Kagame ambao umechezwa Uwanjwa Mkapa na kushuhidiwa na baadhi ya mashabiki ambao walijitokeza pia wengine walishuhudia mubashara kupitia Azam Tv.

Dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu na kugawana pointi mojamoja katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Nyota wao Wazir Junior ambaye ni mshambuliaji amesema kuwa bado wataendelea kupambana ili kupata matokeo kwenye mchezo wao ujao.

Ikumbukwe kwamba mchezo wao uliopita waligawana pointi mojamoja na Big Bullets kwenye mchezo wa ufunguzi ambapo Junior alifunga bao kwa Yanga kwa pasi ya Dickson Ambundo.

Matokeo ya leo yanaifanya Yanga kuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi A na ina pointi 2 vinara ni Express wenye pointi nne ambao mchezo wao wa mwisho watakutana.

6 COMMENTS:

  1. Halafu nyie hii kujiita timu ya wananchi wakati mmejaza wakongo na boss mhindi sijui inatoka wapi

    ReplyDelete
  2. Wananchi hatuna timu ni lazima tukiri. Altabara ni kati ya timu dhaif sana. Tulichokishuhudia ni kama mabio za watoto wadogo wakicheza foliti. Kwa kweli tunaumia.

    ReplyDelete
  3. Hatuna disiplini na hatuwasitahi viongizi. Lini tukisikia wanasinba wanawakashifu na kuwatukana viongizi wao hadharani na hata akitokea mmoja kufanya hivo basi atatengwa na kulaaniwa na wanasimba wote na kujikuta peke yake na kuushia kuomba msahama na hayo tumeshayashudia bila ya kutaja nani au lini

    ReplyDelete
  4. Uto hamna timu munashindwa kufanya vizur kombe la mbuzi je kwenye kombe la ng'ombe itakuaje?

    ReplyDelete
  5. Kama ilivo dasturi ta kulalamika jwa kila wanapokisa ushindi, safari hii kocha wao katika mchezo wa jana na Tabara ya Sudan, analalamika eti Refa kawanyima peneti tano

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic