RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Walles Karia ametangaza kutoa donge nono la sh.milioni kumi kwa Mwenyekiti bora wa chama cha wa mpira ngazi ya mkoa atakayefanya vizuri kuliko wengine baada ya kukidhi vigezo vitakavyowekwa kuwashindanishwa.
Karia
alisema kwa miaka minne aliyoongoza Shirikisho hilo kumekuwepo na changamoto
mbalimbali ikiwemo kutokuwajibika ipasavyo kwa viongozi wanaoongoza vyama vya
mpira wa miguu mikoani ambapo alisema awamu hii hawataki kurudi nyuma tena
watahakikisha wanaimarisha utendaji.
"Ninatangaza
kutoa shilingi milioni kumi kwa Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa atakayefanya
vizuri zaidi kushinda wengine, tutakwenda kuandaa vigezo ambavyo tutavitumia
kumpata mshindi lengo la kufanya ushindani huu ni kuongeza ufanisi kwa
watendaji ili kuweza kuinua mchezo huu,” alisema Karia.
Aliongeza kuwa: “Sisi
shirikisho tuna mahusiano mazuri na
wizara yenye dhamana ya michezo lakini huko mikoani na wilayani hakuna mahusiano
mazuri kati ya vyama vya siasa na
viongozi wa Serikali, niwaombe kujenga ukaribu zaidi ili tuwe katika
mstari mmoja kuliendeleza soka letu la Tanzania,” alisema Karia.
Mara Baada
ya kutangazwa kuwa Rais, Karia
ametangaza Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri hiyo mmoja wapo ni Mwanamama
Hawa Mniga ambaye pia alitia nia ya
kugombea katika nafasi ya Urais wa Shirikisho.








Mheshimiwa hebu angalia uwezekano wa kupunguza wachezaji wageni kwenye ligi zetu, soka letu litaporomoka kwa wachezaji wa kitanzania
ReplyDeleteWatafute nafasi nao Wakacheze nje
Delete