August 9, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeeleza kuwa sababu kubwa ya kuachana na nyota zao wawili ambao ni makipa ni kufuata ripoti ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Ni Metacha Mnata na Faroukh Shikalo ambao wote kandarasi zao zilikuwa zimemeguka na Nabi hakuwa tayari kuona wakiongezewa mkataba.

Kwa mujibu wa Haji Mfikirwa, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa ilikuwa ni mapendekezo ya kocha kuachana na wachezaji hao wote wawili.

"Tunafanya kazi kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu hivyo ni yeye ambaye alipendekeza tufanye hivyo na hakuna namna nyingine.

"Mnata yeye amepewa barua leo ya kuwa mchezaji huru hivyo tunamtakia kila la kheri pamoja na Shikalo," amesema.

14 COMMENTS:

  1. Binafsi nimesikitishwa kwa kuachwa kwa Faroukh Shikalo lakini si kwa yule muuza duka

    ReplyDelete
  2. Na usajili wa Ajibu nao ni ushauri wa kocha Nasridine? Kamuona wapi akicheza? Acheni kuwazuga watu. Kwa Metacha mmepoteza bonge moja la Goal keeper. Timu Kama biashara wanapaswa kumdaka Metacha juujuu. Pia Metacha Hana Cha kupoteza wanaomsimia wajaribu kumtafutia timu nje japo madaraja ya chini kwenye nchi zilizo songa mbele kimpira hata hapa Africa.

    ReplyDelete
  3. Wameshindwa kuambakisha shikalo kwani watakua na ma golikipa wawili wa kigeni. Kwa Metacha yeye ni sawasawa kuachwa, hilo lilikua ni duka la Simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Achana na mawazo finyu, Simba ndo walikuwa wanamtumia bila kumlipa?

      Delete
    2. Kama Haji Manara

      Delete
  4. Mjiandae kusajili kipa mwingine dirisha dogo la sivyo mtajuta

    ReplyDelete
  5. Swala la usajili kinawahusu Yanga, wengine fanyeni yenu

    ReplyDelete
  6. Hata huyo Kocha Nabi achunguzwe

    ReplyDelete
  7. Ama huyo Faruku anatia huruma. Juu ya kiwango kikubwa alichokionesha na mapenzi yake makubwa kwa yanga na kuwa ni yeye ndie aliefsnikisha usajili wa huyo Khalid wa Uganda na kuonesha chuki zake kwa Simba, lakini yote hayo hayakumsaidia kitu, kangolewa kama jino bovu bila ya kupigwa shindano

    ReplyDelete
  8. Safi sana kuacha na dukanla rejareja aka Mechata Mnata, sasa waliokuwa wanamnunua wamsajili na ndio itakuwa funzo kwa vijana wengine. SHIKALO aliomba mwenyewe kuondoka ila pia kwa muda ameshindwa kuwa mwepesi hasa akichunguliwa any way will miss you Shikalo umefanya mazuri Yanga.

    ReplyDelete
  9. Hata huyo mpya ni duka la Simba Kama unabisha subiri septemba 25

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani mukoko atapewa kadi nyekundu tena?

      Delete
    2. Akicheza judo baada ya kuzidiwa soka anapewa haki yake

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic