DICKSON Ambundo, kiungo mshambuliaji ndani ya Yanga amesema kuwa imani yao ni kuweza kufanya vizuri katika men zao za Kagame pamoja na mashindano ya ligi.
Ambundo ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo aliibuka hapo akitokea ndani ya Klabu ya Dodoma Jiji na amepewa dili la miaka miwili.
Katika mchezo wao wa kwanza wa Kagame mbele ya Big Bullets waligawana pointi mojamoja kwa kufunga bao 1-1, Uwanja wa Mkapa.
Nyota huyo amesema:"Kila kitu kinakwenda sawa na tunaamini kwamba tutafanya vizuri kwa mechi ambazo tutacheza kikubwa ni juhudi.
."Mashabiki watupe sapoti tuna amini tutafanya vizuri. Kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi na kazi bado inaendelea, " amesema.
Leo Yanga itakuwa na mchezo dhidi ya Atlabara Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.
Atlabara ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Express kwa kufungwa bao moja kwa bila hivyo leo ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Yanga.
Manji karejea ughaubuni, jee zigo ataliweza mtu mmoja?
ReplyDelete