August 29, 2021


 TIMU gazeti la Spoti Xtra, leo imegawa tiketi kwa wasomaji wake kwa ajili ya kuingia kwenye siku ya Wananchi inayofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar.


Zoezi hilo liliongozwa na Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Juma Johanes na kuwaacha mashabiki hao wakifurahia uhondo wa Spoti Xtra na stori za kutosha. 

Katika zoezi hilo timu ya Spoti Xtra ilipofika Uwanjani hapo ilianza kugawa kwa wasomaji wake iliyowakuta na gazeti hilo.

Kikosi hicho kilizungumza na wasomaji hao na kuwauliza maswali kuhusiana na gazeti Spoti Xtra pamoja na magazeti mengine yanayotolewa na Global Publishers ambapo waliojibu vizuri walijizolea tiketi hizo.

Magazeti mengine yanayotolewa na Global Publishers ni pamoja na Championi, Ijumaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic