BAADA ya kuweza kusonga mbele katika hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho, benchi la ufundi la Azam FC limeweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kufanya vizuri katika mechi yao ijayo dhidi ya Pyramids FC ambao ni Waarabu kutoka Misri.
Mchezo wao wa raundi ya kwanza katika Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 15-17 mwaka huu 2021, Uwanja wa Azam Comple na ule wa marudio utapigwa nchini Misiri.
Azam inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imewaondoa Horseed FC ya Somalia katika Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa jumla ya mabao 4-1 kwa kuwa mchezo wa awali Azam FC ilishinda mabao 3-1 na ule wa marudiano Horseed ilifungwa bao 1-0.
Akizungumza na Saleh Jembe, Vivier Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa baada ya kutoka hapo mipango yao ni kuelekea katika mechi yao dhidi ya Prymids FC.
"Bado kazi haijaisha kwani tunaendelea na mashindano na tuna kazi nyingine ya kufanya mbele ya wapinzani wetu, kikubwa ni kuona kwamba katika mechi zetu ambazo zinakuja tunapata ushindi na kufikia malengo yetu ambapo tunahitaji kuona tunafika hatua ya makundi.
"Hautaweza kufika katika hatua hiyo ikiwa hakuna mpango wa kushinda mechi za mbele kwa kuanzia lazima yale makosa ambayo tumeyafanya katika mechi zilizopita tunayafanyia kazi," amesema Bahati.
Azam chama langu naiombea ipite Tena ha
ReplyDeletetua hiyo