September 20, 2021


 IKIWA ni Septemba 25, wanatarajia kukutana, Uwanja wa Mkapa watani wa jadi Simba v Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, tambo zimeanza kutawala kwa timu zote mbili zikiwa zinahitaji kusepa na taji hilo.


Ni Simba ambao walitwaa Ngao ya Jamii msimu ulioyeyuka wa 2020/12 kwa ushindi mbele ya Namungo wameweka wazi kuwa wanahitaji kutetea taji hilo kama ilivyo kawaida jambo ambalo limejibiwa na mabosi wa Yanga.

Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba aliliambia Championi Jumatatu kuwa mpango mkubwa ni katika kutwaa mataji yote ambayo waliyatwaa msimu uliopita ikiwa ni pamoja na Ngao ya Jamii.

"Tunahitaji kuonyesha kwamba tunauwezo na nguvu ipo katika kutimiza yale tuliyopanga kwa vitendo, tunahitaji kutwaa Ngao ya Jamii, taji la ligi na mengine yote ambayo tutashiriki kikubwa ni kufanya vizuri na tupo tayari, " alisema Mangungu.


Kwa upande wa Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara alisema kuwa kwa namna ambavyo wamesajili wanahitaji kuchukua kila kikombe ikiwa ni pamoja na taji la Ngao ya Jamii.

5 COMMENTS:

  1. Na kombe la kwanza klabu bingwa Africa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba tunakwenda kupiga kwenye mshono wa jeraha la ligi ya mabingwa kisha tunanyunyuzia ndimu.

      Delete
  2. Tulisema yanga itacheza mechi ya ngao ya hisani ikiwa imeshatupwa nje ya kinyang'anyiro cha klabu bingwa Africa, na mechi hii watapigwa.

    ReplyDelete
  3. Kombe la pili ngao ya jamii.

    ReplyDelete
  4. Yanga wanajua sana sijui wanakosea wapi?msimu huu wameanza mapema sana kupigania ubingwa wa makombe na tayari wanaonekana kufanikiwa maana tayari klabu bingwa afrika washabeba,ngao ya jamii tarehe 25 wanabeba,na ligi pia watachukua,ahsante yanga,asante gsm,asante wananchi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic