VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Horseed FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex wakiwa na kazi ya kufanya ambayo ni kusaka ushindi.
Azam FC ina kibarua cha kulinda ushindi wake wa awali wa mabao 3-1 uliopatikana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ambao ni wa Kombe la Shirikisho.
Unachezwa leo saa 10:00 jioni Uwanja wa Azam Complex kwa sababu za Horseed FC ya Somalia imeomba iwe hivyo kutokana na masuala ya kiusalama.
Bahati amesema:"Mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wetu nao wanahitaji matokeo kama ambavyo nasi tunahitaji ushindi.
"Kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya na wachezaji wanajua hilo hivyo ni suala la kusubiri na kuona kwa kuwa malengo ni kusonga mbele," amesema.
Jana kikosi hicho kilifanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo huku wachezaji wao wote wakiwa katika hali ya morali wakiongozwa na Bruce Kangwa, Nicolas Wadada, Mudhathir Yahya.
0 COMMENTS:
Post a Comment