September 18, 2021

OFISA Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa wanakwenda kwenye mchezo mgumu dhidi ya Rivers United ambao unatarajiwa kuchezwa Septemba 19 nchini Nigeria.

 Manara amesema kuwa wamejipanga kupata matokeo na wanaamini kwamba watafanikiwa. Mchezo huo ni wa marudio kwa kuwa ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 0-1 Rivers United hivyo kazi kubwa kwa Yanga ni kwenda kupindua meza kibabe.

 Tayari kikosi cha Yanga kimeshawasili nchini Nigeria kwa ndege binafsi ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic