September 15, 2021


 NAHODHA na beki wa kati wa Azam FC, Aggrey Morris ameibuka na kusema kuwa kwa sasa akili na malengo yao yapo katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Horseed ya Somalia na si kwa Pyramids ya Misri.

 Azam imefanikiwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya Horseed katika mchezo wa kwanza hatua ya awali kwenye Kombe la Shirikisho katika mchezo uliopigwa Jumamosi kabla ya mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa Septemba 18, mwaka huu.

 

Akizungumza na Championi JumatatuMorris alisema kuwa bado wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanafuzu hatua inayofuata kwa kuwa hawapaswi kuwabeza wapinzani wao ambao wameonyesha upinzani mkubwa hivyo haitokuwa rahisi kuwafikiria Pyramid watakaocheza nao kwenye hatua ya pili.

 

“Unajua hii michuano siyo rahisi kwa sababu watu huenda wakaichukulia Horseed ni timu nyepesi kwa kuwa imetoka Somalia lakini kwetu bado ni mechi ngumu ambayo tunahitaji ushindi hivyo ni jukumu la kila mchezaji kuhakikisha anapambana ili tuweze kusonga mbele.

 

“Kiukweli kwa sasa ni ngumu kuweza kuwafuatilia au kuwafikiria Pyramids kwa kuwa bado hatujamaliza hatua hii ingawa kila mtu anajua timu itakayopita hapa itaenda kukutana na Pyramids ila kwa sasa ni jambo ambalo hatuwezi kulipa nafasi,” alisema Morris.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic