September 1, 2021


 MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC na Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya DTB FC ambayo msimu ujao itacheza Championship.

 

Tambwe alitambulishwa hivi karibuni kuwa mchezaji wa DTB ambapo ataungana na mastaa wengine kama Juma Abdul, David Mwantika na Yannick Bazola ili kukiimarisha kikosi hicho kilichopania kucheza Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.


Pia nyota mwingine ambaye amesaini dili jipya kuitumikia timu hiyo ni pamoja na Yusuph Mlipili na Nicholas Gyan ambaye naye aliwahi kucheza Simba. 

 

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTB FC, Muhibu Kanu, amesema: “Maandalizi mpaka sasa yapo vizuri na tumemsajili Tambwe na nyota wengine, hadi sasa timu tayari ipo kambini ikiendelea na mazoezi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar, ambao pia tutautumia kama uwanja wetu wa nyumbani kwenye ligi.

 

“Tumekwisha maliza kusajili na mpaka sasa tuna wachezaji 26 ambao kati yao wachezaji sita ni wa kigeni, mpango wetu kwa sasa ni kuhakikisha tunafanikiwa kufika ligi kuu.”




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic