September 7, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa msimu wa 2021/22 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hesabu zao ni kufika hatua ya makundi.

Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Rivers United ambao utachezwa Uwanja wa Mkapa.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara ameweka wazi kuwa wanatambua itakuwa kazi kubwa lakini lazima wapambane kufikia malengo hayo.

'Malengo yetu makubwa ni kuona kwamba tunaweza kufikia hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kwenye mchezo wetu dhidi ya Rivers United tupo tayari," amesema.

Leo Manara amepokewa na Wazee wa Yanga makao makuu, Jangwani na kuwashukuru kwa jambo hilo alilofanyiwa.

"Wazee wanapokewa na vijana lakini kwa umaalumu ambao mmenifanyia leo nina deni zito, sijawahi kupata na pongezi kwa wazee kwa hili walilofanya.

"Deni hili ninalo kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kwa namna ambavyo tumefanya nao kazi juzi kwenye mechi yetu, hivyo deni hili halina budi kulipwa kwa nguv, kufanya kazi kwa kujitoa sana, kwa mapenzi na uadilifu mkubwa kwa klabu ambayo nilianza kucheza hapa," amesema Manara.

1 COMMENTS:

  1. Nauliza tena, hivi ni tayari manara mi msemaji wa yanga?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic