September 20, 2021


 IMEELEZWA kuwa Cedrick Kaze aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga atarejea ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi.

Kaze alikuwa ndani ya Yanga msimu uliomeguka wa 2020/21 ambapo hakuweza kukamilisha mzunguko wa pili baada ya mabosi wa timu hiyo kuamua kumfungashia virago.

Kwa mujibu wa Yanga walieleza kuwa Kaze alishindwa kuwapa kile ambacho walikuwa wanafikiria jambo ambalo liliwafanya waweze kufikia makubaliano ya kuachana naye.

Mechi yake ya mwisho alishuhudia vijana wake wakigawana pointi mojamoja dhidi ya Polisi Tanzania na bao la Yanga lilifungwa na mchezaji Fiston Abdulazak ambaye kwa sasa hayupo ndani ya kikosi hicho.

Taarifa zimeeleza kuwa Kaze anarejea Yanga akiwa ni kocha msaidizi huku Kocha Mkuu akibaki kuwa Nasreddine Nabi.


Alipotafutwa Kaze ili aweze kuzungumzia jambo hilo hakuwa tayari kufunguka ishu ilivyo.

15 COMMENTS:

  1. Hiyo timu ni ya wanayanga tunaumia kwa uendeshwaji wa klabu yetu viongozi mnatia mashaka Kama ni nyinyi ni wananchi halisi tatizo media zinabrand timu Sana wakt performance iko chini inauma Sana kuona timu mbovuu cjui tunafeli wapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mikakati ya viongozi wa Yanga ni kuifunga simba CAF hawana habari icho ndo pasua kichwa cha yanga

      Delete
  2. Scoutting ya wachezaji haiko makini Kuna wachezaji inapaswa wameondoke cz performance iko chini Kama adeyun,nchimbi always hamtaki ukweli bt football inaonekana uwanjan

    ReplyDelete
  3. Manara ANA KAZI NGUMU SANA YA KUONGELEA USHINDI USIOWEZA KUPATIKANA NA KUONGELEA UBINGWA USIOWEZA KUPATIKANA

    ReplyDelete
  4. Huwa KAMPUNI IKIWA HAILETI FAIDA INALETA HASARA INAWEZA KUUZWA SASA KWANINI YANGA ISIUZWE KWA MO ???

    ReplyDelete
  5. Sasa naona mnazidi kujivuruga almuradi nasi pia tuwe na makocha watatu

    ReplyDelete
  6. Silaha kubwa iliobaki ni kupiga makelele ya kuonewa nyumbani na ughaibuni

    ReplyDelete
  7. Hawa wadudu wa msimbazi wanaandika nini kwenye mambo ya Yanga? Achieni Wananchi wapambane na hali yao. Mwandishi anatuka habari za kukamata tu majinga. Yanga ipo vizuri subiri kidogo mtajua

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba wanaongea sana kuzima habar za tiktaka kwa mkapa siku ua tamasha lao, eti kwa mkapa hatoki mtu, tuliwaambia lengo la tamasha ni kutambulisha wachezaj wapya je vitu vimo,, walitucheka eti tumefungwa, mara nao wakadunguliwa hali ikawa kimyaaaa

      Delete
    2. Tena pyaaaaaaaaaaaaaaaa! Ziiiiiiiiii!

      Delete
    3. Bongo mko poa, Kenya ndiyo ovyo!!

      Delete
  8. Mimi nachoomba Wana yanga au viongoz wa yanga mtu mvumilie kocha nabi Mana ndo kwanza ananza kufufua kikosi cha Wana yanga kwoo tunaitaj uvumilivu wa hali ya juu..hakuna ngoja isiyo andaliwa..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic