September 3, 2021


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kimezidi kujiimarisha kwa ajili ya msimu mpya wa 2021/22.

Baada ya kufanikiwa kufanya tamasha lao la Wiki ya Mwananchi, Agosti 29, Uwanja wa Mkapa nguvu kubwa zimeelekezwa katika msimu mpya.

Awali kambi yao iliyowekwa Morocco ilivunjwa kwa kile ambacho kilielezwa kuwa ni sababu muhimu kwa maslahi mapana ya timu hivyo wanaendelea na kambi wakiwa kwenye kijiji cha Avic Town, Kigamboni.

Kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Zanaco waliruhusu ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 1-2 Zanaco jambo ambalo lilibainishwa na Kocha wa Makipa wa Yanga, Razack Siwa kwamba wameona mapungufu watayafanyia kazi.

Pia jana waliweza kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na watupiaji walikuwa ni Ditram Nchimbi, Fiston Mayele na Yusuph Umamwiko. 

3 COMMENTS:

  1. Huyu nchimbi sidhani kama ana uwezo bado wa kutumikia timu inayopambana kimataifa nashangaa tuu bado yupo yanga

    ReplyDelete
  2. Ni bora kutafuta timu zenye mana kuliko vitimu vidogo almuradi muwe mmeshinda ikumbukwe mnakwenda kupanbana na timu zenye majina

    ReplyDelete
  3. Inabidi Yanga iwebigwa msimu ujao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic